Sunday, January 20, 2019

Mwezi mkubwa mwekundu kuonekana duniani


Mwezi mkubwa mwekundu
Watu kote duniani wanatarajiwa kuona kupatwa kwa mwezi utakaobadilika na kuwa mwekundu .
Wakati wa kupatwa kwa mwez,i dunia hutoa kivuli chekundu.
Kupatwa huko kwa mwezi kutaonekana kutoka kaskazini na Kusini mwa Marekani pamoja na maeneo ya magharibi mwa Ulaya ikiwemo Uingereza na kaskazini mwa Afrika

Kupatwa kwa mwezi ni nini?

Tukio hili hujiri wakati dunia inapopita katikati ya Jua na mwezi.
Katika hali hii, jua huwa nyuma ya dunia huku mwezi ukizunguka katika kivuli cha dunia.

Je mwezi mwekundu ni upi?

Maelzo ya mwezi mwekundu
Presentational white space

Je mwezi huo utakuwa mwekundu?

Ndio. Baadhi ya watangazaji huuita "super blood wolf moon".
Jina "super" linatokana na ukweli kwamba mwezi huo utakuwa karibu sana na dunia ambapo utaonekana kuwa mkubwa angani zaidi ya kawaida.
Nalo Jina "wolf" linatokana na majina yanayopewa miezi mikubwa mwezi Januari "wolf moons".
Walter freeman , naibu profesa katika chuo kikuu cha Syracuse University mjini New York state, alisema: "mwanga mdogo wa jua hutolewa na dunia na kufika katika mwezi, ukijipinda kando kando ya dunia.
Kiwango hiki cha rangi nyekundu huangazia mwezi vya kutosha kwa binadamu kuweza kuona.

Wapi na lini nitauona mnwezi huo?

Kupatwa kwa mwezi kutaanza mwendo wa 02:35 GMT siku ya Monday na kukamilika katika saa 07:49 GMT, lakini kipindi ambacho mwezi wote utakuwa mwekundu kitakuwa mwendo wa 05:12 GMT.
Nchini Uingereza mwezi utakuwa juu ya upeo wa macho katika kipindi chote cha kupatwa kwa mwezi ijapokuwa kusini mashariki mwa Uingereza, jua litaonekana kupaa huku luna hiyo ikikamilika.
Kupatwa huko kutaonekana kaskazini magharibi mwa Ufaransa, kaskani magharibi mwa Uhispania, Ureno, na eneo dogo la Afrika magharibi, karibu eneo lote la kaskazni na Amerika Kusini, mashariki mwa Pacific pamoja na kilele cha Ksakzini mashairiki mwa Urusi.

Je ni salama kuutazama?

Huku matukio ya kupatwa kwa mwezi yakitajwa kuwa hatari kutazama moja kwa moja, mwangaza wa kupatwa kwa mwezi ni mdogo hivyobasi ni salama kutazama bila kutumia vifaa vyovyote.

Je ina muhimu gani?

Tukio hilo ni la mwisho kwa watazamaji wa anga nchini Uingereza kuona kupatwa kwa mwezi kwa kipindi cha muda mrefu hadi 2029- hali ya hewa itakaporuhusu.

Thursday, July 21, 2016

KUELEKEA MKUTANO WA CCM KINANA AONGEA

Kinana atoa Masharti Endapo Rais Magufuli Atamhitaji Aendelee Kuwa Katibu Mkuu wa CCM

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ametoa neno endapo Rais John Magufuli atamhitaji kuendelea na wadhifa huo, huku akibainisha kuwa amekutana na changamoto nyingi katika nafasi hiyo kiasi kwamba wakati mwingine alikata tamaa.

Mwanasiasa huyo maarufu ndani ya CCM na nchini, anatarajiwa kuhitimisha uongozi wake wiki hii wakati Mwenyekiti mpya wa CCM Taifa, Rais John Magufuli atakapokabidhiwa uenyekiti huo na kuunda Sekretarieti yake mpya ambayo haijulikani kama itaongozwa tena na Kanali huyo wa zamani wa Jeshi.

Akizungumza jana na waandishi wa habari baada ya kukagua Ukumbi wa Mkutano Maalumu wa CCM utakaofanyika keshokutwa Jumamosi, Kinana ambaye amekuwa katika nafasi hiyo kwa miaka mitatu na nusu, alisema aliombwa katika nafasi hiyo baada ya kuwa aliamua kustaafu, lakini akakumbana na changamoto mbalimbali.

CCM kuwa mbali na wananchi 
Alisema kuna wakati aliona kama vile chama kiliacha kwenda kwa wananchi na kwamba hakikuwa karibu sana nao.

“Ninyi ni mashahidi, ikabidi kubuni utaratibu mzuri wa kwenda kwa wananchi ili chama kiwe karibu na wananchi, kiwasikilize na kuwa sauti ya wananchi kifuatilie matatizo yao kisimamie utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi,” alisema Kinana na kuongeza kuwa katika kufanya hivyo amekuwa akiwasiliana na Rais na Waziri Mkuu kwa ajili ya matatizo kutatuliwa.

“Changamoto ya pili ya kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya chama, hapo nyuma kulikuwa na misukosuko kidogo ya umoja na mshikamano, kushutumiana na kulaumiana,” alisema na kuongeza kuwa kazi nyingine aliyofanya ni kuimarisha umoja ndani ya chama, kushirikiana na viongozi wenzake kuhakikisha chama kinajitahidi kwa kadri ya uwezo wake kurejea katika misingi yake ya awali katika maeneo ya uadilifu, uwajibikaji na utendaji kazi kwa ufanisi.

Azuiwa ziarani
Kinana alisema amekwenda wilaya zote, majimbo, mikoa na nusu ya kata za nchi na amesafiri zaidi ya kilometa 192,000, kufanya mikutano zaidi ya 3,700 ya aina mbalimbali ya ndani na nje na haikuwa kazi rahisi

 “Changamoto nilizokutana nazo ambazo lazima nikiri ni pale nilipotaka wakati mwingine kufanya ziara kwenye maeneo fulani fulani niliambiwa ni hatarishi siwezi kwenda kwa hiyo ilibidi nibishane na viongozi na watendaji wakuu wa serikali…nikasema hapana nimeamua kwenda lazima niende,” alisema Kinana.

Katibu huyo akitoa mfano alisema kuna wakati aliamua kutoka kwa boti kutoka Nyamisati wilayani Rufiji kwenda Mafia, viongozi wa Mkoa wa Pwani walifikiri si njia salama ya kusafiri na kumpelekea ujumbe asisafiri kwa boti, bali asafiri kwa ndege, lakini alisema hapana ataondoka kwa boti.

“Walichofanya wakakaa kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na wakaniandikia barua rasmi kwamba tunakushauri usisafiri kwa boti safiri kwa ndege kwa maana nyingine walikuwa wanajivua lawama kwa yatakayotokea, lakini vile vile kunitisha kidogo kwamba si salama zaidi nikawasisitiza hapana,” alieleza Kinana.

Ashitakiwa kwa JK
“Baadaye Rais mstaafu Kikwete alikuwa Msoga, viongozi wa Mkoa wa Pwani wakaenda kumwambia tumezungumza na Katibu Mkuu wako naona hasikii tumemuandikia barua ya kumuomba asisafiri na boti hasikii, Rais akaandika meseji ndefu sana…nikamjibu rais nakuheshimu mamlaka yako ni makubwa si vizuri nikakukatalia, lakini niruhusu nikukatalie kwa sababu hata wananchi wanaosafiri kwenye boti hii wanahatarisha maisha yao, ni vizuri na mimi nikahatarisha maisha yangu hata kidogo… akaniambia nimekuelewa endelea,” alibainisha.

Alisema zipo changamoto nyingi sana nyingine, kwa mfano Mbambabay kwenda Kyela, mkuu wa mkoa akamuambia boti haifai kusafiri akasema mara haiwezi kusafiri imeharibika.

“Nikazungumza na Mwakyembe akapeleka mafundi wakatengeneza, safari haikuwa rahisi, lakini changamoto zilikuwa nyingi sana, kwingine Lupingu kule ni gari moja tu ndio inayoshuka chini hakuna kupishana magari nikaambiwa nisiende nikasema nina kwenda,” alisema na kuongeza kuwa kulikuwa na ubishi mwingi wakati mwingine alionekana mtu mmoja kidogo ambaye hasikilizi ushauri sana.

Pia nyingine zinazotokana na changamoto za wananchi kutolipwa mazao yao kwa wakati, mbolea kutofika kwa wakati, halmashauri kutopata fedha za maendeleo kwa wakati, watumishi wa umma wanaohamishwa kwenda vijijini hawaendi vijijini kwenda kuwahudumia wananchi, tatizo kubwa la migogoro kati ya wakulima na wafugaji kati ya wananchi na hifadhi za taifa.

“Ndio maana mnaniona siku hizi nimenyamaza kwa sababu yale yote niliyokuwa nikiyaombea yanafanyika, umangimeza haupo watu wachape kazi wawahudumie wananchi, uadilifu unapigwa vita, rushwa inapigwa vita, uwajibikaji na uadilifu unahimizwa, utendaji kazi unatakiwa na hayo yasipofanyika mtu anaondolewa mara moja,” alifafanua Kinana ambaye kuanzia mwaka 2014 hadi mwanzoni mwa mwaka jana alitembea kote nchini akikisafisha chama chake na kuibana serikali.

Kurejea kwake CCM
“Yalitokea mazingira ambayo niliombwa na viongozi wastaafu na viongozi wa chama kuniomba niwe mtendaji mkuu wa chama chetu. Si nafasi ambayo niliipenda, bali niliitwa na nikakalishwa wakanisihi na mimi nikakubali sababu ni wito na kwa kuwa ni watu ninaowaheshimu na wana dhamana kubwa kwenye nchi yetu, nikakubali kufanya kazi hiyo,” alisema Kinana akizungumzia jinsi alivyoteuliwa kushika nafasi hiyo.

Alisema amekuwepo katika uongozi ndani ya chama kwa muda mrefu (miaka 25) ndani ya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa, na alihisi ni wakati muafaka wa kung’atuka.

“Mwanasiasa mzuri ni yule anayejua wakati wa kuingia na wakati wa kutoka. Ni wakati mzuri wa kung’atuka kuachia waingie wenye umri wa kati na umri wa vijana kuachia waongoze chama na kuwaamini,”alieleza.

Alisema moja ya mambo ambayo walikubaliana wakati ule akajitahidi kukiimarisha chama, kusimamia na kumsaidia mwenyekiti kusimamia mchakato wa kuwapata wagombea kwenye nafasi zote za Urais, Ubunge na Udiwani. Pia alijitahidi kuendesha shughuli za kampeni na uchaguzi na utakamalizika.

“Uchaguzi umekwisha niruhusiwe kupumzika, na wote waliafiki na kukubali sasa muda umefika kwa hiyo nimewakumbusha yale tuliyokubaliana muda wake umefika sasa wengine wakaniuliza hivi ndivyo tulivyokubaliana nikawaambia wazee hamjawa wazee kiasi cha kusahau ndio haya tuliyokubaliana,” alieleza.

Akiombwa na JPM
Alipoulizwa kama akiombwa na Rais Magufuli aendelee kwa Katibu Mkuu, Kinana alisema, “Niseme hajasema, hatujazungumza hilo, likitokea tutaangalia, tutakaa naye kikao kama akiniomba, tutakuwa na kikao na mazungumzo muda utakapofika kama nilivyokuwa na mazungumzo na kikao kama kwa wale walioniomba mwaka 2012.”

Waliokisaliti chama
Akizungumzia walioisaliti CCM katika Uchaguzi Mkuu mwaka jana, mtendaji huyo wa CCM alisema msaliti yeyote adhabu yake ni mbaya sana, hata kwenye chama cha siasa.

“Kwenye CCM wapo watu walioyumba, kulikuwa na wimbi kubwa mwaka jana, watu waliyumba hivi kidogo wakakaa mguu upande huku hawapo na kule hawapo, wako ambao sio tu waliyumba, bali walikiuka maadili na hawakushiriki kwenye shughuli za kampeni,” alisema.

Pia alisema wapo ambao hawakushiriki, hawakusaidia na wakasaidia upinzani na kila mtu atakuwa na adhabu yake kulingana na makosa yake.

“Kama mmekuwa mkifuatilia kuna waliochukuliwa hatua ngazi za wilaya na mikoa. Kwa mfano, Shinyanga 123 walichukuliwa hatua. Wapo wanaotakiwa kuchukuliwa hatua kwenye ngazi za juu, sasa jambo moja mtu yeyote kabla ya kuchukuliwa hatua lazima aelezwe mashtaka yake, apewe fursa ya kusikilizwa, kwa hiyo hawa wote watasomewa mashtaka, watasikiliza na kupewa adhabu kwa kadri itakavyostahili, lakini hatua zitachukuliwa mara baada ya Mkutano Mkuu kumalizika,”alieleza.

LOWASA ANENA YA ROHONI

Lowassa Ataka Mbowe alindwe kama nyuki wanavyomlinda malkia wao

ALIYEKUWA mgombea urais kupitia mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa amewataka vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumlinda Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kama nyuki wanavyomlinda malkia wao.

Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alitoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha Kamati ya Utendaji ya Baraza la Vijana (Bavicha) jijini Dar es Salaam jana.

Waziri mkuu huyo wa zamani, pamoja na mambo mengine aliwataka vijana wa chama hicho kuacha vita vya ndani kwa ndani na badala yake washikamane na kuwang’ang’ania viongozi wanaowaongoza.

“Tuache vita vya ndani kwa ndani, Mbowe ndiye mwenyekiti wetu wa chama…tumlinde kama nyuki wanavyomlinda malkia wao. Mtu akishakuwa kiongozi tumg’ang’anie,”alisema Lowassa.

Lowassa ambaye alijiunga na upinzani mwishoni mwa mwaka jana alisema kumekuwapo na kawaida ya kuibuka kwa makundi uchaguzi unapomalizika.

Azungumzia uchumi
Katika mkutano huo, Lowassa pia alizungumzia uchumi ambapo alisema hivi sasa maisha ya Watanzania walio wengi hayana uhakika, huku matumaini kidogo yakielekezwa kwa watu wachache.

“Binadamu anaishi kwa matumaini, lakini mambo yanayoendelea hapa nchini hayatoi matumaini hayo…hali ya uchumi inakwenda vibaya sana, kuna rafiki yangu mmoja ana msamiati wake anasema maisha ni pasua kichwa hivi sasa kwa sababu hayana uhakika,” alisema Lowassa.

Aidha Lowassa alieleza kusikitishwa kwake kwa baadhi ya watu kuacha kuzikana kwa sababu ya siasa ambapo alisema hayo ni mambo ya ovyo.

Ajivunia vijana
Katika hotuba yake hiyo, Lowassa aliwapongeza Bavicha kwa kutii maelekezo ya Mbowe kuhusu kusitisha uamuzi wao wa kwenda Dodoma kuzuia Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Niwapongeze kwa kutii maelekezo ya mwenyekiti wetu, najua haikuwa rahisi, mlikuwa mmeshajipanga lakini maelekezo ya mwenyekiti ni mazuri, vitu vingine si lazima uende mbali sana ni kama kwenye simu kwamba ‘message sent’ mlifikisha ujumbe mahsusi hata kama hawakubaliani lakini ujumbe umefika.

“Wala msione aibu mnachofanya, vijana mngefanya tofauti ningeshangaa, nyie ndio chachu ya mabadiliko lazima mje na kitu kipya na mawazo mapya, ninyi ni jeshi la chama.

“Kwa uzoefu wangu CCM lazima watakwenda kumtambulisha mwenyekiti wao mpya katika Uwanja wa  Jamhuri mjini Dodoma, hivyo wananchi wenyewe wataangalia na kupima kama Chadema wanazuiwa kwa nini wapinzani wazuiwe, waachane wapate tabu kujieleza kwa umma” alisema Lowassa huku akishangiliwa.

Kuhusu uteuzi uliofanywa na Rais John Magufuli hivi karibuni, Lowassa aliuponda na kusema ni wa kibaguzi kwa sababu umewatenga vijana wa vyama vya upinzani.

“Kama wewe ni CCM utakuwa mkuu wa wilaya, mkoa na hata mkurugenzi wa halmashauri lakini hali ni tofauti kwa vijana wa upinzani, wanabaguliwa utadhani si Watanzania.

“Hili ni jambo la kutafakari na kukemea kwa sabu ajira ni tatizo hapa nchini, lakini hata hizo chache zinatoka kwa kubaguana pamoja na jitihada zote lakini hazisaidii,”alisema.

MAKAMU MWENYEKITI WA CHAMA CHA NCCR MAGEUZI ATIMULIWA

Thursday, July 21, 2016

NCCR wamtimua makamu Mwenyekiti wa Chama

Chama cha NCCR – Mageuzi kimemvua uanachama makamu mwenyekiti wake (Bara), Leticia Ghati (pichani) kikimtuhumu kujihusisha na migogoro ndani ya chama na tuhuma nyingine za kijinai. 

Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa uamuzi huo umepitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho. 

Mbunge huyo wa Vunjo na mwenyekiti mwenza wa Ukawa, alisema makosa mengine aliyokutwa nayo Ghati ni pamoja na kukashifu na kutoa tuhuma dhidi ya kiongozi wa chama nje ya utaratibu na kuhujumu chama wakati wa uchaguzi. 

“Kwa makosa hayo ambayo Leticia Ghati aliyatenda wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2015 Halmashauri Kuu ya Taifa, inamsimamisha uongozi na kumvua uanachama,” alisema Mbatia. 

Mustakabali wa chama 
Akizungumzia mustakabali wa chama hicho katika Ukawa, Mbatia alisema Halmashauri Kuu ya chama hicho itaendelea kusimama imara kuhakikisha umoja huo unakuwa bora na taifa linapata Katiba kama yalivyokuwa malengo ya kuanzishwa kwake. 

“NCCR tutahakikisha Ukawa unaboreka na kusimama imara kwa ajili ya kupata Katiba, tumeazimia kuunga mkono jitihada za kuunganisha vyama vinavyounda umoja huu ili kufikia lengo la kuwa na chama kimoja cha siasa chenye nguvu,” alisema Mbatia. 

Mbatia pia alizungumzia hali ya kisiasa na kidemokrasia nchini na kusema chama chake kimebaini kuwa taifa linaongozwa kwa matamko ya Rais John Magufuli badala ya kufuata Katiba, sheria na kanuni.

Alisema demokrasia imeendelea kukiukwa huku uhuru wa kujieleza ukiendelea kudidimizwa na akatolea mfano mwenendo wa Bunge ambao alisema licha ya kuwa chombo cha kikatiba chenye mamlaka kamili ya kujiendesha, limeanza kuingiliwa katika uendeshaji wake kwa wabunge kunyimwa fursa ya kujadili kwa uwazi masuala ya Watanzania. 

Alisema NCCR inakemea matu- mizi ya nguvu za dola kupitia Jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, kuwakamata na kuwaweka rumande viongozi wa kisiasa na kuwashtaki kwa makosa mbalimbali. 

“NCCR Mageuzi tunalaani tabia ya polisi kuwakamata na kuwahoji mara kwa mara viongozi wa kisiasa na kuwashtaki kwa makosa mbalimbali… vitendo hivi ni ukiukaji wa uhuru na haki za vyama vya siasa katika kufanya kazi zao,” alisema Mbatia.

gharama ya tcu na namna ya kulipia 2016

How to Apply
Applications shall be done through Internet. Applicants should not submit their applications to TCU by e-mail, fax, or deliver them in person. NB: Applicants should ensure that they have paid the application fee through prescribed procedures before starting application.
7.1. Payment Details
7.1.1. How to pay via MaxMalipo agents (Only those applying using Form Six qualifications and should pay to TCU):
Steps
1. Visit the nearest Maxmalipo agent with your Tshs 50,000/-
2. The agent will take your cash and request for your mobile phone number.
3. The agent will process your payment and issue you a receipt that contains a voucher number.
4. You will shortly receive an SMS as well as a voucher number.
 Use the voucher number as payment ID for registration to apply on TCU Central Admission System (CAS).
7.1.2. How to pay via M-Pesa
Steps
1. Dial *150*00#
2. Select option # 4: Pay via M-PESA
3. Select option #4: Enter Business number: 240077
Undergraduate Admission Guidebook for Higher Education Institutions in Tanzania for Applicants with Form
Six and RPL Qualifications 2016/2017
8
4. Enter payment reference number: 123456
5. Enter Amount: 50,000/-
6. Enter your PIN
7. Enter 1 to confirm
 You will receive an M-PESA notification SMS confirming your transaction.
 You will then receive another SMS from TCU with voucher Number that you can use as Payment ID on the Central Admission System (CAS) for registration
7.1.3. How to pay via Tigo_Pesa
Steps
1. Dial *150*01#
2. Select option # 4: PayBill
3. Select option #2 to enter the Business number
4. Enter the Business number:240077
5. Enter reference of payment: 123456
6. Enter amount: Tshs 50,000/-
7. Enter your PIN
 You will receive a Tigopesa notification SMS confirming your transaction.
 You will then receive another SMS from TCU with voucher number that you can use as Payment ID on the Central Admission System (CAS) for registration

tcu online registration 2016


http://cas.tcu.go.tz/users/selfregister/1

Friday, July 15, 2016

samwel sita amehamishwa nyumba ya serikali


SeeBait
ALIYEKUWA Spika wa Bunge la tisa, Samuel Sitta, ameondolewa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi baada ya Serikali kugoma kumlipia kodi ya pango.

Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania, mwanasiasa huyo mashuhuri, aliondolewa katika nyumba hiyo iliyopo Masaki, Dar es Salaam na kulazimika kuanza kuhamisha vyombo vyake tangu Ijumaa ya Julai 8, mwaka huu.

Kwa muda wote tangu akiwa Spika wa Bunge, Serikali ilikuwa inalipa kiasi cha dola 8,000 ambazo ni sawa na zaidi ya Sh milioni 12 kwa ajili ya nyumba hiyo.

Sitta ambaye baadaye alikuwa waziri katika Wizara ya Afrika Mashariki pamoja na Uchukuzi, aliendelea kuishi katika nyumba hiyo kwa nafasi yake.

Kwa mujibu wa kijana aliyekuwa nyumbani hapo, alisema walianza kuhama tangu mwishoni mwa wiki iliyopita na wanaendelea kuhama kwa kuhamisha vitu kidogo kidogo.

“Ni kweli mzee amehama hapa, tangu Ijumaa tulikuwa tunahamisha vyombo taratibu na sijui kama Serikali imegoma kulipa kodi ama la, ila sasa amehamia jirani tu hapo Mtaa wa Manzese, hapa hapa Masaki.

“Nasikia nyumba imepata mpangaji mpya ndiyo maana wanahama,”alisema.

Alipotafutwa Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bunge, Owen Mwandumbya, ili kuzungumzia hilo, alimtaka mwandishi kuwatafuta Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Wizara ya Fedha.

Alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa utaratibu wa malipo kwa maspika wastaafu, ikiwa ni pamoja na matunzo na nyumba wanazoishi, Owen alisema Bunge halihusiki na stahiki zozote za wastaafu kwa mujibu wa sheria.

“Watafute Utumishi na Wizara ya Fedha, wao ndio wahusika, Ofisi ya Bunge haihusiki na stahiki zozote za wastaafu kwa mujibu wa sheria, isipokuwa Utumishi na Wizara ya Fedha ndio wahusika,” alisema.

Alipotafutwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, alisema hana taarifa hizo za kuondolewa kwa Sitta hivyo atafuatilia.

Hata hivyo, alipotafutwa tena kupitia simu yake ya kiganjani, Kairuki alimtaka mwandishi kuwatafuta Hazina, kwamba ndio wanaoweza kulisemea jambo hilo.

“Naomba uwatafute Hazina wakupe ufafanuzi, halafu baadaye urudi kwangu,” alisema Kairuki.

Alipotafutwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kupitia simu yake ya kiganjani, ili kupata ufafanuzi wa suala hilo, alisema:“Ufafanuzi kuhusu malipo kwa viongozi wastaafu unatolewa kwa viongozi husika na si kwa vyombo vya habari.”

Hali hiyo ya Sitta, imekuwa ni tofauti na aliyekuwa Spika wa Bunge la 10, Anne Makinda, ambaye Serikali kupitia Bunge iligharimia matengenezo ya nyumba yake iliyoko Kijitonyama, Dar es Salaam, ambako ujenzi wake ulikumbana na lawama kali za wananchi wanaoishi jirani na eneo hilo.

Spika Makinda alilaumiwa na majirani zake kwa kusababisha usumbufu baada ya kuziba njia inayopita katika eneo hilo kwenda maeneo ya Sinza.

Kwa mujibu wa Margaret Sitta ambaye ni mke wa Samweli Sitta na  Mbunge wa Urambo, alisema kuwa walikuwa wakiishi kwenye nyumba hiyo ya Serikali kwa kuwa mumewe alikuwa Waziri wa Uchukuzi, lakini Baraza la Mawazili lilivunjwa tangu mwaka jana hivyo walipaswa kuhama.

Chanzo: Mtanzania

shule kumi bora matokeo kidato cha sita 2016

Seebait.com 2016

NECTA Imezitaja Shule 10 Bora Kitaifa Pamoja na Shule 10 za Mwisho Kitaifa

SeeBait
Baraza la mitihani Tanzania(NECTA) imetangaza matokeo ya kidato cha sita 2016, na Kuzitaja shule zilizo fanya vizuri zaidi Kitaifa na zile ambazo hazikufanya vizuri Kitaifa.

Ubora wa shule umepagwa kwa kutumia kigezo cha Wastani wa Pointi(Grade Point Average – GPA) ambapo A=1, B=2, C=3, D=4, E=5 na F=7

Aidha, upangaji wa shule zilizofanya vizuri umezingatia shule zenye idadi ya watahiniwa wasiopungua 30 kama ifuatavyoa:

==>Shule 10 Bora Kitaifa
1. Kisimiri (Government)

2. Feza Boys (Private)

3. Mwanza Alliance Girls (Private)

4. Feza Girls (Private)

5. Tabora Boys (Government)

6. Marian Boys (Private)

7. Kibaha (Government)

8. Mzumbe (Government)

9. Ilboru (Government)

10. Tandahimba (Private)


==>Shule 10  za  Mwisho Kitaifa
1.Mpendae (Unguja)

2.Ben bella ( Unguja)

3.Tumekuja (Unguja) 

4.Green Bird Boys (Kilimanjaro)

5.Jang'ombe (Unguja )

6.Kiembesamaki (Unguja ) 

7.Tanzania Adventist ( Arusha )

8.Al-Ihsan Girls ( Unguja )

9.Azania (Dar es salaam )

10: Lumumba (Unguja) 

NECTA 2016 VYUO VYA UALIMU

MFUMO WA KUTUNUKU MATOKEO KIDATO CHA SITA BOFYA HAPA
http://www.necta.go.tz/view_news?id=125
MATOKOE YA UALIMU DSEE
http://tanzania.go.tz/result_acsee_2016/DSEE2016/index.htm
 http://41.188.136.75/results2016/DSEE2016/index.htm 
GATCE http://tanzania.go.tz/result_acsee_2016/GATCE2016/index.htm
GATCE http://41.188.136.75/results2016/GATCE2016/index.htm
KIDATO CHA SITA
http://41.188.136.75/results2016/ACSEE2016/index.htm

MATOKEO KIDATO CHA SITA 2016

BOFYA HAPA
http://tanzania.go.tz/result_acsee_2016/ACSEE2016/index.htm

Tuesday, July 12, 2016

diamond ft p square official video

click hapa kuupakua http://www.djmwanga.com/2016/07/official-video-diamond-platnumz-ft.html

Serikali Yakunjua Makucha.....Yakamata mali za kampuni ya Uingereza zenye thamani ya Dola mil 500

Tuesday, July 12, 2016

SeeBait
Seebait.com 2016

SERIKALI imeiamuru Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuzishikilia akaunti za Kampuni kubwa ya mafuta ya Uingereza (BG Group) hadi pale itakapolipa Kodi ya Ongezeko la Mtaji (capital gain tax) yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 502.

Taarifa zilizoandikwa na gazeti moja la wiki, TRA tayari imetoa maelekezo kwa Benki ya Citi kushikilia akaunti za kampuni hiyo.

TRA inadai kiasi hicho kutokana na faida iliyotokana na BG Group kuziuza hisa zake asilimia 60 kwa kampuni nyingine za nishati za Royal Dutch Shell, Exxon Mobil, Ophir Energy na Statoil.

Biashara hiyo, pia ilihusisha maslahi ya BG, visima vya mafuta namba 1 na 4 vilivyopo kusini mwa Tanzania.

Vyanzo vya habari kutoka Wizara ya Fedha na TRA, vilisema amri hiyo imetolewa kushikilia akaunti za BG Group hadi kodi hiyo itakapolipwa.

Baada ya akaunti kukaguliwa, ilibainika fedha zilizopo katika benki hiyo, ni Dola milioni 5 tu, ikiwa ni sawa na asilimia moja tu ya kiasi inachodai TRA.

Uamuzi huo unazua maswali katika rufaa, ambayo  BG Group imeifungua katika Mahakama ya Kodi Tanzania ikipinga namna tathimini ilivyofanyika kupata kiasi hicho inachodaiwa.

BG Group, inasema haiwezi kulipa kodi kwa sababu iliwekeza Dola milioni 850 ya jumla ya faida iliyopata katika visima Tanzania.

BG Group iliendelea kudai kampuni yake dada, tayari imetumia dola bilioni 1.5 kama uwekezaji, na hivyo kuashiria upotevu wa mtaji.

Kwa mujibu wa Sheria ya Rufaa ya Kodi ya Mapato (2006), mtu yeyote asiyeridhishwa na kiasi cha kodi anachodaiwa anaweza kupinga kwa kumuandikia Kamishina Mkuu.

Ibara ya 12 (3) ya sheria hiyo inasema. “Wakati taarifa ya kupinga kiasi cha kodi kinachodaiwa inapowasilishwa, mtu anayepinga anatakiwa wakati akisubiri uamuzi wa mwisho wa Kamishina Mkuu kwa mujibu wa Ibara ya 13, alipe kiasi cha kodi ambacho hakikupingwa au theluthi moja ya kiasi kilichopingwa, bila kujali ukubwa wa kiwango”.

Lakini wanasheria na wataalamu wa nishati, wameitaka Serikali na BG Group kutatua mkwamo huo, ambao unaweza kuchelewesha uamuzi wa mwisho wa uwekezaji wa dola milioni 30 wa mradi wa usindikaji wa gesi ya asili ya matumizi mbalimbali (LNG), ambao kampuni hiyo ina mipango ya kuijenga kwa ubia na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Ujenzi huo wa mtambo wa LNG, utakaozalisha tani milioni 10 za gesi kwa mwaka, awali ulikuwa ukamilike mwaka 2020.

Lakini chini ya sheria za nchi, ujenzi hauwezi kupitishwa hadi kodi itakapolipwa kwanza.

Serikali imebakia kimya kuhusu suala hilo, lakini Kamishina Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata alisema suala hilo bado halijafika kwake, huku Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akilitaka gazeti hilo kumuuliza Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Dk. James Mataragio, ambaye hakuwa tayari kusema lolote.

Kuna wasiwasi mizozo kuhusu kodi inaweza kuathiri uwekezaji wa kigeni unaotarajiwa kuwekezwa nchini.

Wachambuzi wa mambo wanaamini kampuni ya Shell kupitia hisa BG, imejipanga kimkakati kujipatia vibali vya utafutaji wa mafuta Zanzibar kwa sasa kwa vile inamiliki pamoja na Serikali. Shell imekuwa ikihaha kwa miaka 10 sasa kujipatia vibali vya utafutaji mafuta visiwani humo.

Subiro Mwapinga, mshauri katika kampuni ya ushauri wa masuala ya gesi na mafuta ya Mnazi Bay Consulting Group, alisema mzozo wa sasa wa kodi umeuweka uwekezaji wa LNG katika hatari na unaweza kuathiri miradi mingine, ikiwamo ujenzi wa pipa la mafuta baina ya Uganda hadi Tanga wenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 10.

“Iwapo ukokotoaji wa kodi wa TRA umefanywa kwa kufuata taratibu zote za kimataifa na kuendana na sheria, kuna nafasi ndogo kwa BG Group kuweza kukwepa kulipa kodi, lakini bado hilo lina athari zake linapokuja suala la kubadilisha miundo ya mradi wa LNG, ambayo imepangwa kujengwa kwa ubia na washirika mbalimbali.

Kwa mfano, linaweza kusababisha washirika wengine kujenga miradi yao wenyewe ya LNG,” anasema Mwapinga.

Vyanzo vya habari ndani ya Wizara ya Fedha na TRA vilisema serikali pia imeamua kwa muda kusimamisha maombi ya Shell na BG Group ya kufufua vibali vya kutafiti nishati katika visima viwili hadi mgogoro huo utakapomalizika.

Kibali cha kisima namba 1 kinaishia Desemba mwaka huu, huku cha kisima namba 4 kikiishia Oktoba 2017.

Vibali vya kutafuta mafuta hutolewa kwa kipindi cha miaka minne kisha kufufuliwa kwa miaka minne mingine na kisha kipindi kingine cha miaka mitatu, baada ya hapo kampuni inatarajia kuomba kibali cha uendelezaji.

Kisha kwa mujibu wa kumbukumbu za serikali, kampuni itaongezewa wastani wa chini wa miaka 11 na kuomba vibali vya maendeleo lakini haiko tayari bado kwa hilo.

“Hali hiyo inaonesha Shell inatakiwa kuomba kuongezwa muda kwa kibali cha kutafuta mafuta kwa ajili ya kisima namba 1 na  4, lakini ongezo la muda huwa chini ya mamlaka ya waziri kwa vile liko nje ya kipindi cha miaka 11.  Ni hapo serikali ndiyo iliyoshikilia mpini,” vyanzo vya habari vilisema.

Mbunge wa Karagwe, Innocent Bashungwa (CCM) na mratibu wa zamani wa Taasisi ya Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji Tanzania,alisema usimamizi wa sekta ya mafuta na gesi unahusisha mabilioni ya dola za uwekezaji na miamala mbalimbali katika shughuli za hapa na pale.

“Wakati kunapotokea mabadiliko, migogoro inaweza kuibuka iwapo mfumo wa sheria wa nchi husika hauko wazi kuhusu taratibu za miamala,” alisema Bashungwa.

Mbunge huyo alisema, migogoro ni ishara ya udhaifu wa kisheria na maandalizi ya taratibu. “Naamini Serikali na BG zitapata suluhu kwa amani kwa fedha hizo za ongezeko la mtaji zinazobishaniwa.

“Vinginevyo wanachama wa Chama cha Mafuta na Gesi Tanzania na wawekezaji watarajiwa watalichukulia kama kengele ya hatari ya kitakachowatokea siku za usoni,” alisema mbunge huyo.

Rais Magufuli aagiza vyombo vya Serikali kuanza kutumia mashine za EFD

Tuesday, July 12, 2016

Rais Magufuli aagiza vyombo vya Serikali kuanza kutumia mashine za EFD.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk John Pombe Magufuli amewaagiza makatibu wakuu kuhakikisha vyombo vyote vinavyokusanya mapato serikalini vinatumia mashine za kielekrtoniki (EFD).
 
Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akizungumza na wakurugenzi wateule wa Halmashauri,Wilaya,Majiji na Manispaa Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi hao wa umma.
 
“Vyombo vya Serikali lazima vianze kutumia mashine za EFD,haiwezekani  wafanyabiashara wawe na mashine za EFD alafu maafisa wa serikali hawana,kama tumeamua kwenda kwa elektroniki lazima twende hivyo”Alisema Rais Magufuli.
 
Aidha amewataka wakurugenzi  wote kuchukua mashine hizi na kwenda nazo katika maeneo yao ya kazi ili ziwasaidie katika ukusanyaji wa mapato ya serikali katika halmshauri zao.
 
Pia amewaagiza wakurugenzi hao kukusanya kodi na kutatua kero za wananchi wa chini zisizokuwa na lazima na kuongezea kuwa kama watakuta watendaji wa chini yao wasioendana  na kasi ya awamu ya tano basi watumie madaraka yao kuwaweka sawa.
 
Rais magufuli pia amewaagiza wakurugenzi hao kusimamia ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi kwakuwa waliahidi kutatua kero za wananchi na wahakikishe wanazitatua ili wananchi waishi vizuri kwa amani ndani ya nchi yao na kuongezea kuwa viongozi wa juu wana imani kubwa sana nao ndio maana hata wakachaguliwa kutoka katika watanzania hawa milioni 50.
 
Aidha Rais magufuli amewataka wakurugenzi hao kusimamia kuanzishwa kwa viwanda vidogo vidogo katika maeneo yao ili kukamilisha azma ya serikali ya awamu ya tano ya kuwa na viwanda.

Mbali na hayo pia amewataka wakurugenzi hao kubadilika kifikra na kuachana na kuongoza kwa historia kwani wananchi wa sasa wamebadilika na hivyo wafanye kazi kwa bidii ili kuwatimizia wananchi yale wanayotaka na hivyo nchi itasonga mbele.

DOKTA MWAKA AFUNGIWA

Tuesday, July 12, 2016

Kituo Cha Dk. Mwaka Chafutiwa Usajili Wake


Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, limekifutia usajili wake wa kutoa huduma za kitabu, Kituo cha Tiba Asilia cha ForePlan Kliniki kilichopo Ilala Bungoni jijini Dar es salaam, kinachomilikiwa na Dkt. Juma Mwaka maarufu kama Dkt. Mwaka, kwa madai kuwa kimekiuka taratibu za kitabu za tiba mbadala.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dkt. Edmund Kayombo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ukumbi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Habari kwa kina baadae.