Thursday, July 21, 2016

KUELEKEA MKUTANO WA CCM KINANA AONGEA

Kinana atoa Masharti Endapo Rais Magufuli Atamhitaji Aendelee Kuwa Katibu Mkuu wa CCM

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ametoa neno endapo Rais John Magufuli atamhitaji kuendelea na wadhifa huo, huku akibainisha kuwa amekutana na changamoto nyingi katika nafasi hiyo kiasi kwamba wakati mwingine alikata tamaa.

Mwanasiasa huyo maarufu ndani ya CCM na nchini, anatarajiwa kuhitimisha uongozi wake wiki hii wakati Mwenyekiti mpya wa CCM Taifa, Rais John Magufuli atakapokabidhiwa uenyekiti huo na kuunda Sekretarieti yake mpya ambayo haijulikani kama itaongozwa tena na Kanali huyo wa zamani wa Jeshi.

Akizungumza jana na waandishi wa habari baada ya kukagua Ukumbi wa Mkutano Maalumu wa CCM utakaofanyika keshokutwa Jumamosi, Kinana ambaye amekuwa katika nafasi hiyo kwa miaka mitatu na nusu, alisema aliombwa katika nafasi hiyo baada ya kuwa aliamua kustaafu, lakini akakumbana na changamoto mbalimbali.

CCM kuwa mbali na wananchi 
Alisema kuna wakati aliona kama vile chama kiliacha kwenda kwa wananchi na kwamba hakikuwa karibu sana nao.

“Ninyi ni mashahidi, ikabidi kubuni utaratibu mzuri wa kwenda kwa wananchi ili chama kiwe karibu na wananchi, kiwasikilize na kuwa sauti ya wananchi kifuatilie matatizo yao kisimamie utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi,” alisema Kinana na kuongeza kuwa katika kufanya hivyo amekuwa akiwasiliana na Rais na Waziri Mkuu kwa ajili ya matatizo kutatuliwa.

“Changamoto ya pili ya kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya chama, hapo nyuma kulikuwa na misukosuko kidogo ya umoja na mshikamano, kushutumiana na kulaumiana,” alisema na kuongeza kuwa kazi nyingine aliyofanya ni kuimarisha umoja ndani ya chama, kushirikiana na viongozi wenzake kuhakikisha chama kinajitahidi kwa kadri ya uwezo wake kurejea katika misingi yake ya awali katika maeneo ya uadilifu, uwajibikaji na utendaji kazi kwa ufanisi.

Azuiwa ziarani
Kinana alisema amekwenda wilaya zote, majimbo, mikoa na nusu ya kata za nchi na amesafiri zaidi ya kilometa 192,000, kufanya mikutano zaidi ya 3,700 ya aina mbalimbali ya ndani na nje na haikuwa kazi rahisi

 “Changamoto nilizokutana nazo ambazo lazima nikiri ni pale nilipotaka wakati mwingine kufanya ziara kwenye maeneo fulani fulani niliambiwa ni hatarishi siwezi kwenda kwa hiyo ilibidi nibishane na viongozi na watendaji wakuu wa serikali…nikasema hapana nimeamua kwenda lazima niende,” alisema Kinana.

Katibu huyo akitoa mfano alisema kuna wakati aliamua kutoka kwa boti kutoka Nyamisati wilayani Rufiji kwenda Mafia, viongozi wa Mkoa wa Pwani walifikiri si njia salama ya kusafiri na kumpelekea ujumbe asisafiri kwa boti, bali asafiri kwa ndege, lakini alisema hapana ataondoka kwa boti.

“Walichofanya wakakaa kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na wakaniandikia barua rasmi kwamba tunakushauri usisafiri kwa boti safiri kwa ndege kwa maana nyingine walikuwa wanajivua lawama kwa yatakayotokea, lakini vile vile kunitisha kidogo kwamba si salama zaidi nikawasisitiza hapana,” alieleza Kinana.

Ashitakiwa kwa JK
“Baadaye Rais mstaafu Kikwete alikuwa Msoga, viongozi wa Mkoa wa Pwani wakaenda kumwambia tumezungumza na Katibu Mkuu wako naona hasikii tumemuandikia barua ya kumuomba asisafiri na boti hasikii, Rais akaandika meseji ndefu sana…nikamjibu rais nakuheshimu mamlaka yako ni makubwa si vizuri nikakukatalia, lakini niruhusu nikukatalie kwa sababu hata wananchi wanaosafiri kwenye boti hii wanahatarisha maisha yao, ni vizuri na mimi nikahatarisha maisha yangu hata kidogo… akaniambia nimekuelewa endelea,” alibainisha.

Alisema zipo changamoto nyingi sana nyingine, kwa mfano Mbambabay kwenda Kyela, mkuu wa mkoa akamuambia boti haifai kusafiri akasema mara haiwezi kusafiri imeharibika.

“Nikazungumza na Mwakyembe akapeleka mafundi wakatengeneza, safari haikuwa rahisi, lakini changamoto zilikuwa nyingi sana, kwingine Lupingu kule ni gari moja tu ndio inayoshuka chini hakuna kupishana magari nikaambiwa nisiende nikasema nina kwenda,” alisema na kuongeza kuwa kulikuwa na ubishi mwingi wakati mwingine alionekana mtu mmoja kidogo ambaye hasikilizi ushauri sana.

Pia nyingine zinazotokana na changamoto za wananchi kutolipwa mazao yao kwa wakati, mbolea kutofika kwa wakati, halmashauri kutopata fedha za maendeleo kwa wakati, watumishi wa umma wanaohamishwa kwenda vijijini hawaendi vijijini kwenda kuwahudumia wananchi, tatizo kubwa la migogoro kati ya wakulima na wafugaji kati ya wananchi na hifadhi za taifa.

“Ndio maana mnaniona siku hizi nimenyamaza kwa sababu yale yote niliyokuwa nikiyaombea yanafanyika, umangimeza haupo watu wachape kazi wawahudumie wananchi, uadilifu unapigwa vita, rushwa inapigwa vita, uwajibikaji na uadilifu unahimizwa, utendaji kazi unatakiwa na hayo yasipofanyika mtu anaondolewa mara moja,” alifafanua Kinana ambaye kuanzia mwaka 2014 hadi mwanzoni mwa mwaka jana alitembea kote nchini akikisafisha chama chake na kuibana serikali.

Kurejea kwake CCM
“Yalitokea mazingira ambayo niliombwa na viongozi wastaafu na viongozi wa chama kuniomba niwe mtendaji mkuu wa chama chetu. Si nafasi ambayo niliipenda, bali niliitwa na nikakalishwa wakanisihi na mimi nikakubali sababu ni wito na kwa kuwa ni watu ninaowaheshimu na wana dhamana kubwa kwenye nchi yetu, nikakubali kufanya kazi hiyo,” alisema Kinana akizungumzia jinsi alivyoteuliwa kushika nafasi hiyo.

Alisema amekuwepo katika uongozi ndani ya chama kwa muda mrefu (miaka 25) ndani ya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa, na alihisi ni wakati muafaka wa kung’atuka.

“Mwanasiasa mzuri ni yule anayejua wakati wa kuingia na wakati wa kutoka. Ni wakati mzuri wa kung’atuka kuachia waingie wenye umri wa kati na umri wa vijana kuachia waongoze chama na kuwaamini,”alieleza.

Alisema moja ya mambo ambayo walikubaliana wakati ule akajitahidi kukiimarisha chama, kusimamia na kumsaidia mwenyekiti kusimamia mchakato wa kuwapata wagombea kwenye nafasi zote za Urais, Ubunge na Udiwani. Pia alijitahidi kuendesha shughuli za kampeni na uchaguzi na utakamalizika.

“Uchaguzi umekwisha niruhusiwe kupumzika, na wote waliafiki na kukubali sasa muda umefika kwa hiyo nimewakumbusha yale tuliyokubaliana muda wake umefika sasa wengine wakaniuliza hivi ndivyo tulivyokubaliana nikawaambia wazee hamjawa wazee kiasi cha kusahau ndio haya tuliyokubaliana,” alieleza.

Akiombwa na JPM
Alipoulizwa kama akiombwa na Rais Magufuli aendelee kwa Katibu Mkuu, Kinana alisema, “Niseme hajasema, hatujazungumza hilo, likitokea tutaangalia, tutakaa naye kikao kama akiniomba, tutakuwa na kikao na mazungumzo muda utakapofika kama nilivyokuwa na mazungumzo na kikao kama kwa wale walioniomba mwaka 2012.”

Waliokisaliti chama
Akizungumzia walioisaliti CCM katika Uchaguzi Mkuu mwaka jana, mtendaji huyo wa CCM alisema msaliti yeyote adhabu yake ni mbaya sana, hata kwenye chama cha siasa.

“Kwenye CCM wapo watu walioyumba, kulikuwa na wimbi kubwa mwaka jana, watu waliyumba hivi kidogo wakakaa mguu upande huku hawapo na kule hawapo, wako ambao sio tu waliyumba, bali walikiuka maadili na hawakushiriki kwenye shughuli za kampeni,” alisema.

Pia alisema wapo ambao hawakushiriki, hawakusaidia na wakasaidia upinzani na kila mtu atakuwa na adhabu yake kulingana na makosa yake.

“Kama mmekuwa mkifuatilia kuna waliochukuliwa hatua ngazi za wilaya na mikoa. Kwa mfano, Shinyanga 123 walichukuliwa hatua. Wapo wanaotakiwa kuchukuliwa hatua kwenye ngazi za juu, sasa jambo moja mtu yeyote kabla ya kuchukuliwa hatua lazima aelezwe mashtaka yake, apewe fursa ya kusikilizwa, kwa hiyo hawa wote watasomewa mashtaka, watasikiliza na kupewa adhabu kwa kadri itakavyostahili, lakini hatua zitachukuliwa mara baada ya Mkutano Mkuu kumalizika,”alieleza.

LOWASA ANENA YA ROHONI

Lowassa Ataka Mbowe alindwe kama nyuki wanavyomlinda malkia wao

ALIYEKUWA mgombea urais kupitia mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa amewataka vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumlinda Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kama nyuki wanavyomlinda malkia wao.

Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alitoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha Kamati ya Utendaji ya Baraza la Vijana (Bavicha) jijini Dar es Salaam jana.

Waziri mkuu huyo wa zamani, pamoja na mambo mengine aliwataka vijana wa chama hicho kuacha vita vya ndani kwa ndani na badala yake washikamane na kuwang’ang’ania viongozi wanaowaongoza.

“Tuache vita vya ndani kwa ndani, Mbowe ndiye mwenyekiti wetu wa chama…tumlinde kama nyuki wanavyomlinda malkia wao. Mtu akishakuwa kiongozi tumg’ang’anie,”alisema Lowassa.

Lowassa ambaye alijiunga na upinzani mwishoni mwa mwaka jana alisema kumekuwapo na kawaida ya kuibuka kwa makundi uchaguzi unapomalizika.

Azungumzia uchumi
Katika mkutano huo, Lowassa pia alizungumzia uchumi ambapo alisema hivi sasa maisha ya Watanzania walio wengi hayana uhakika, huku matumaini kidogo yakielekezwa kwa watu wachache.

“Binadamu anaishi kwa matumaini, lakini mambo yanayoendelea hapa nchini hayatoi matumaini hayo…hali ya uchumi inakwenda vibaya sana, kuna rafiki yangu mmoja ana msamiati wake anasema maisha ni pasua kichwa hivi sasa kwa sababu hayana uhakika,” alisema Lowassa.

Aidha Lowassa alieleza kusikitishwa kwake kwa baadhi ya watu kuacha kuzikana kwa sababu ya siasa ambapo alisema hayo ni mambo ya ovyo.

Ajivunia vijana
Katika hotuba yake hiyo, Lowassa aliwapongeza Bavicha kwa kutii maelekezo ya Mbowe kuhusu kusitisha uamuzi wao wa kwenda Dodoma kuzuia Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Niwapongeze kwa kutii maelekezo ya mwenyekiti wetu, najua haikuwa rahisi, mlikuwa mmeshajipanga lakini maelekezo ya mwenyekiti ni mazuri, vitu vingine si lazima uende mbali sana ni kama kwenye simu kwamba ‘message sent’ mlifikisha ujumbe mahsusi hata kama hawakubaliani lakini ujumbe umefika.

“Wala msione aibu mnachofanya, vijana mngefanya tofauti ningeshangaa, nyie ndio chachu ya mabadiliko lazima mje na kitu kipya na mawazo mapya, ninyi ni jeshi la chama.

“Kwa uzoefu wangu CCM lazima watakwenda kumtambulisha mwenyekiti wao mpya katika Uwanja wa  Jamhuri mjini Dodoma, hivyo wananchi wenyewe wataangalia na kupima kama Chadema wanazuiwa kwa nini wapinzani wazuiwe, waachane wapate tabu kujieleza kwa umma” alisema Lowassa huku akishangiliwa.

Kuhusu uteuzi uliofanywa na Rais John Magufuli hivi karibuni, Lowassa aliuponda na kusema ni wa kibaguzi kwa sababu umewatenga vijana wa vyama vya upinzani.

“Kama wewe ni CCM utakuwa mkuu wa wilaya, mkoa na hata mkurugenzi wa halmashauri lakini hali ni tofauti kwa vijana wa upinzani, wanabaguliwa utadhani si Watanzania.

“Hili ni jambo la kutafakari na kukemea kwa sabu ajira ni tatizo hapa nchini, lakini hata hizo chache zinatoka kwa kubaguana pamoja na jitihada zote lakini hazisaidii,”alisema.

MAKAMU MWENYEKITI WA CHAMA CHA NCCR MAGEUZI ATIMULIWA

Thursday, July 21, 2016

NCCR wamtimua makamu Mwenyekiti wa Chama

Chama cha NCCR – Mageuzi kimemvua uanachama makamu mwenyekiti wake (Bara), Leticia Ghati (pichani) kikimtuhumu kujihusisha na migogoro ndani ya chama na tuhuma nyingine za kijinai. 

Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa uamuzi huo umepitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho. 

Mbunge huyo wa Vunjo na mwenyekiti mwenza wa Ukawa, alisema makosa mengine aliyokutwa nayo Ghati ni pamoja na kukashifu na kutoa tuhuma dhidi ya kiongozi wa chama nje ya utaratibu na kuhujumu chama wakati wa uchaguzi. 

“Kwa makosa hayo ambayo Leticia Ghati aliyatenda wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2015 Halmashauri Kuu ya Taifa, inamsimamisha uongozi na kumvua uanachama,” alisema Mbatia. 

Mustakabali wa chama 
Akizungumzia mustakabali wa chama hicho katika Ukawa, Mbatia alisema Halmashauri Kuu ya chama hicho itaendelea kusimama imara kuhakikisha umoja huo unakuwa bora na taifa linapata Katiba kama yalivyokuwa malengo ya kuanzishwa kwake. 

“NCCR tutahakikisha Ukawa unaboreka na kusimama imara kwa ajili ya kupata Katiba, tumeazimia kuunga mkono jitihada za kuunganisha vyama vinavyounda umoja huu ili kufikia lengo la kuwa na chama kimoja cha siasa chenye nguvu,” alisema Mbatia. 

Mbatia pia alizungumzia hali ya kisiasa na kidemokrasia nchini na kusema chama chake kimebaini kuwa taifa linaongozwa kwa matamko ya Rais John Magufuli badala ya kufuata Katiba, sheria na kanuni.

Alisema demokrasia imeendelea kukiukwa huku uhuru wa kujieleza ukiendelea kudidimizwa na akatolea mfano mwenendo wa Bunge ambao alisema licha ya kuwa chombo cha kikatiba chenye mamlaka kamili ya kujiendesha, limeanza kuingiliwa katika uendeshaji wake kwa wabunge kunyimwa fursa ya kujadili kwa uwazi masuala ya Watanzania. 

Alisema NCCR inakemea matu- mizi ya nguvu za dola kupitia Jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, kuwakamata na kuwaweka rumande viongozi wa kisiasa na kuwashtaki kwa makosa mbalimbali. 

“NCCR Mageuzi tunalaani tabia ya polisi kuwakamata na kuwahoji mara kwa mara viongozi wa kisiasa na kuwashtaki kwa makosa mbalimbali… vitendo hivi ni ukiukaji wa uhuru na haki za vyama vya siasa katika kufanya kazi zao,” alisema Mbatia.

gharama ya tcu na namna ya kulipia 2016

How to Apply
Applications shall be done through Internet. Applicants should not submit their applications to TCU by e-mail, fax, or deliver them in person. NB: Applicants should ensure that they have paid the application fee through prescribed procedures before starting application.
7.1. Payment Details
7.1.1. How to pay via MaxMalipo agents (Only those applying using Form Six qualifications and should pay to TCU):
Steps
1. Visit the nearest Maxmalipo agent with your Tshs 50,000/-
2. The agent will take your cash and request for your mobile phone number.
3. The agent will process your payment and issue you a receipt that contains a voucher number.
4. You will shortly receive an SMS as well as a voucher number.
 Use the voucher number as payment ID for registration to apply on TCU Central Admission System (CAS).
7.1.2. How to pay via M-Pesa
Steps
1. Dial *150*00#
2. Select option # 4: Pay via M-PESA
3. Select option #4: Enter Business number: 240077
Undergraduate Admission Guidebook for Higher Education Institutions in Tanzania for Applicants with Form
Six and RPL Qualifications 2016/2017
8
4. Enter payment reference number: 123456
5. Enter Amount: 50,000/-
6. Enter your PIN
7. Enter 1 to confirm
 You will receive an M-PESA notification SMS confirming your transaction.
 You will then receive another SMS from TCU with voucher Number that you can use as Payment ID on the Central Admission System (CAS) for registration
7.1.3. How to pay via Tigo_Pesa
Steps
1. Dial *150*01#
2. Select option # 4: PayBill
3. Select option #2 to enter the Business number
4. Enter the Business number:240077
5. Enter reference of payment: 123456
6. Enter amount: Tshs 50,000/-
7. Enter your PIN
 You will receive a Tigopesa notification SMS confirming your transaction.
 You will then receive another SMS from TCU with voucher number that you can use as Payment ID on the Central Admission System (CAS) for registration

tcu online registration 2016


http://cas.tcu.go.tz/users/selfregister/1