Tuesday, July 12, 2016
diamond ft p square official video
click hapa kuupakua http://www.djmwanga.com/2016/07/official-video-diamond-platnumz-ft.html
Serikali Yakunjua Makucha.....Yakamata mali za kampuni ya Uingereza zenye thamani ya Dola mil 500
Tuesday, July 12, 2016
SERIKALI
imeiamuru Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuzishikilia akaunti za
Kampuni kubwa ya mafuta ya Uingereza (BG Group) hadi pale itakapolipa
Kodi ya Ongezeko la Mtaji (capital gain tax) yenye thamani ya Dola za
Marekani milioni 502.
Taarifa zilizoandikwa na gazeti moja la wiki, TRA tayari imetoa maelekezo kwa Benki ya Citi kushikilia akaunti za kampuni hiyo.
TRA
inadai kiasi hicho kutokana na faida iliyotokana na BG Group kuziuza
hisa zake asilimia 60 kwa kampuni nyingine za nishati za Royal Dutch
Shell, Exxon Mobil, Ophir Energy na Statoil.
Biashara hiyo, pia ilihusisha maslahi ya BG, visima vya mafuta namba 1 na 4 vilivyopo kusini mwa Tanzania.
Vyanzo
vya habari kutoka Wizara ya Fedha na TRA, vilisema amri hiyo imetolewa
kushikilia akaunti za BG Group hadi kodi hiyo itakapolipwa.
Baada
ya akaunti kukaguliwa, ilibainika fedha zilizopo katika benki hiyo, ni
Dola milioni 5 tu, ikiwa ni sawa na asilimia moja tu ya kiasi inachodai
TRA.
Uamuzi
huo unazua maswali katika rufaa, ambayo BG Group imeifungua katika
Mahakama ya Kodi Tanzania ikipinga namna tathimini ilivyofanyika kupata
kiasi hicho inachodaiwa.
BG Group, inasema haiwezi kulipa kodi kwa sababu iliwekeza Dola milioni 850 ya jumla ya faida iliyopata katika visima Tanzania.
BG
Group iliendelea kudai kampuni yake dada, tayari imetumia dola bilioni
1.5 kama uwekezaji, na hivyo kuashiria upotevu wa mtaji.
Kwa
mujibu wa Sheria ya Rufaa ya Kodi ya Mapato (2006), mtu yeyote
asiyeridhishwa na kiasi cha kodi anachodaiwa anaweza kupinga kwa
kumuandikia Kamishina Mkuu.
Ibara
ya 12 (3) ya sheria hiyo inasema. “Wakati taarifa ya kupinga kiasi cha
kodi kinachodaiwa inapowasilishwa, mtu anayepinga anatakiwa wakati
akisubiri uamuzi wa mwisho wa Kamishina Mkuu kwa mujibu wa Ibara ya 13,
alipe kiasi cha kodi ambacho hakikupingwa au theluthi moja ya kiasi
kilichopingwa, bila kujali ukubwa wa kiwango”.
Lakini
wanasheria na wataalamu wa nishati, wameitaka Serikali na BG Group
kutatua mkwamo huo, ambao unaweza kuchelewesha uamuzi wa mwisho wa
uwekezaji wa dola milioni 30 wa mradi wa usindikaji wa gesi ya asili ya
matumizi mbalimbali (LNG), ambao kampuni hiyo ina mipango ya kuijenga
kwa ubia na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Ujenzi huo wa mtambo wa LNG, utakaozalisha tani milioni 10 za gesi kwa mwaka, awali ulikuwa ukamilike mwaka 2020.
Lakini chini ya sheria za nchi, ujenzi hauwezi kupitishwa hadi kodi itakapolipwa kwanza.
Serikali
imebakia kimya kuhusu suala hilo, lakini Kamishina Mkuu wa TRA, Alphayo
Kidata alisema suala hilo bado halijafika kwake, huku Waziri wa Nishati
na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akilitaka gazeti hilo kumuuliza
Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Dk. James Mataragio, ambaye hakuwa tayari
kusema lolote.
Kuna wasiwasi mizozo kuhusu kodi inaweza kuathiri uwekezaji wa kigeni unaotarajiwa kuwekezwa nchini.
Wachambuzi
wa mambo wanaamini kampuni ya Shell kupitia hisa BG, imejipanga
kimkakati kujipatia vibali vya utafutaji wa mafuta Zanzibar kwa sasa kwa
vile inamiliki pamoja na Serikali. Shell imekuwa ikihaha kwa miaka 10
sasa kujipatia vibali vya utafutaji mafuta visiwani humo.
Subiro
Mwapinga, mshauri katika kampuni ya ushauri wa masuala ya gesi na
mafuta ya Mnazi Bay Consulting Group, alisema mzozo wa sasa wa kodi
umeuweka uwekezaji wa LNG katika hatari na unaweza kuathiri miradi
mingine, ikiwamo ujenzi wa pipa la mafuta baina ya Uganda hadi Tanga
wenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 10.
“Iwapo
ukokotoaji wa kodi wa TRA umefanywa kwa kufuata taratibu zote za
kimataifa na kuendana na sheria, kuna nafasi ndogo kwa BG Group kuweza
kukwepa kulipa kodi, lakini bado hilo lina athari zake linapokuja suala
la kubadilisha miundo ya mradi wa LNG, ambayo imepangwa kujengwa kwa
ubia na washirika mbalimbali.
Kwa mfano, linaweza kusababisha washirika wengine kujenga miradi yao wenyewe ya LNG,” anasema Mwapinga.
Vyanzo
vya habari ndani ya Wizara ya Fedha na TRA vilisema serikali pia
imeamua kwa muda kusimamisha maombi ya Shell na BG Group ya kufufua
vibali vya kutafiti nishati katika visima viwili hadi mgogoro huo
utakapomalizika.
Kibali cha kisima namba 1 kinaishia Desemba mwaka huu, huku cha kisima namba 4 kikiishia Oktoba 2017.
Vibali
vya kutafuta mafuta hutolewa kwa kipindi cha miaka minne kisha
kufufuliwa kwa miaka minne mingine na kisha kipindi kingine cha miaka
mitatu, baada ya hapo kampuni inatarajia kuomba kibali cha uendelezaji.
Kisha
kwa mujibu wa kumbukumbu za serikali, kampuni itaongezewa wastani wa
chini wa miaka 11 na kuomba vibali vya maendeleo lakini haiko tayari
bado kwa hilo.
“Hali
hiyo inaonesha Shell inatakiwa kuomba kuongezwa muda kwa kibali cha
kutafuta mafuta kwa ajili ya kisima namba 1 na 4, lakini ongezo la muda
huwa chini ya mamlaka ya waziri kwa vile liko nje ya kipindi cha miaka
11. Ni hapo serikali ndiyo iliyoshikilia mpini,” vyanzo vya habari vilisema.
Mbunge
wa Karagwe, Innocent Bashungwa (CCM) na mratibu wa zamani wa Taasisi ya
Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji
Tanzania,alisema usimamizi wa sekta ya mafuta na gesi unahusisha
mabilioni ya dola za uwekezaji na miamala mbalimbali katika shughuli za
hapa na pale.
“Wakati
kunapotokea mabadiliko, migogoro inaweza kuibuka iwapo mfumo wa sheria
wa nchi husika hauko wazi kuhusu taratibu za miamala,” alisema Bashungwa.
Mbunge huyo alisema, migogoro ni ishara ya udhaifu wa kisheria na maandalizi ya taratibu. “Naamini Serikali na BG zitapata suluhu kwa amani kwa fedha hizo za ongezeko la mtaji zinazobishaniwa.
“Vinginevyo
wanachama wa Chama cha Mafuta na Gesi Tanzania na wawekezaji watarajiwa
watalichukulia kama kengele ya hatari ya kitakachowatokea siku za
usoni,” alisema mbunge huyo.
Rais Magufuli aagiza vyombo vya Serikali kuanza kutumia mashine za EFD
Tuesday, July 12, 2016
Rais Magufuli aagiza vyombo vya Serikali kuanza kutumia mashine za EFD.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk John Pombe Magufuli
amewaagiza makatibu wakuu kuhakikisha vyombo vyote vinavyokusanya mapato
serikalini vinatumia mashine za kielekrtoniki (EFD).
Rais
Magufuli ameyasema hayo wakati akizungumza na wakurugenzi wateule wa
Halmashauri,Wilaya,Majiji na Manispaa Ikulu jijini Dar es Salaam wakati
wa kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi hao wa umma.
“Vyombo
vya Serikali lazima vianze kutumia mashine za EFD,haiwezekani
wafanyabiashara wawe na mashine za EFD alafu maafisa wa serikali
hawana,kama tumeamua kwenda kwa elektroniki lazima twende hivyo”Alisema
Rais Magufuli.
Aidha
amewataka wakurugenzi wote kuchukua mashine hizi na kwenda nazo katika
maeneo yao ya kazi ili ziwasaidie katika ukusanyaji wa mapato ya
serikali katika halmshauri zao.
Pia
amewaagiza wakurugenzi hao kukusanya kodi na kutatua kero za wananchi
wa chini zisizokuwa na lazima na kuongezea kuwa kama watakuta watendaji
wa chini yao wasioendana na kasi ya awamu ya tano basi watumie madaraka
yao kuwaweka sawa.
Rais
magufuli pia amewaagiza wakurugenzi hao kusimamia ilani ya uchaguzi ya
chama cha mapinduzi kwakuwa waliahidi kutatua kero za wananchi na
wahakikishe wanazitatua ili wananchi waishi vizuri kwa amani ndani ya
nchi yao na kuongezea kuwa viongozi wa juu wana imani kubwa sana nao
ndio maana hata wakachaguliwa kutoka katika watanzania hawa milioni 50.
Aidha
Rais magufuli amewataka wakurugenzi hao kusimamia kuanzishwa kwa
viwanda vidogo vidogo katika maeneo yao ili kukamilisha azma ya serikali
ya awamu ya tano ya kuwa na viwanda.
Mbali
na hayo pia amewataka wakurugenzi hao kubadilika kifikra na kuachana na
kuongoza kwa historia kwani wananchi wa sasa wamebadilika na hivyo
wafanye kazi kwa bidii ili kuwatimizia wananchi yale wanayotaka na hivyo
nchi itasonga mbele.
DOKTA MWAKA AFUNGIWA
Tuesday, July 12, 2016
Kituo Cha Dk. Mwaka Chafutiwa Usajili Wake
Baraza
la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, limekifutia usajili wake wa kutoa
huduma za kitabu, Kituo cha Tiba Asilia cha ForePlan Kliniki kilichopo
Ilala Bungoni jijini Dar es salaam, kinachomilikiwa na Dkt. Juma Mwaka
maarufu kama Dkt. Mwaka, kwa madai kuwa kimekiuka taratibu za kitabu za
tiba mbadala.
Hayo
yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dkt. Edmund Kayombo
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ukumbi wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Habari kwa kina baadae.
Subscribe to:
Posts (Atom)