Saturday, January 26, 2019

JINSI YA KUPATA UTAJIRI
Imeandaliwa na
Hassan Issa Khamis
hansb2269@gmail.com

Kila mtu anahitaji kuwa tajiri na matajiri wanahitaji kuendelea kuwa matajiri katika maisha yao, lakini ni watu wachache sana waonajua wafanye nini ili waweze kuwa matajiri. Kuwa tajiri huchukua mchanganyiko wa mambo matatu,
·         Bahati,
·         Ujuzi na
·         Uvumilivu. 
Vile vile utahitajika kujiweka kwenye mambo yanayoopelekea kupata faida, kutumia fedha unazopata kwa busara kwa kuziwekeza, kuzihifadhi, na kupunguza gharama zako za maisha. Kupata utajiri si rahisi, lakini ukiwa na uvumilivu na ujuzi wa kufanya maamuzi, ni dhahiri inawezekana.
NJIA YAKWANZA: UWEKEZAJI
Wekeza fedha zako kwenye hifadhi itakupa faida kwa kila mwaka kwenye uwekezaji (ROI). Kwa mfano, ukiwekeza milioni mbili katika taasisi yenye riba 7%, utapata faida ya 140,000. Maelezo kuhusu soko la hisa bonyeza linki hapo chini.
2.      Usiekeze biashara ya muda mrefu. 
Watu wengine wanajihusisha katika biashara yenye faida ya haraka, ambapo mwisho wa siku biashara ushindwa kuendelea, kuishia kudaiwa fedha na taasisi za fedha au watu pamoja na kuweka rehani mali zao. Watu wanapenda kufanya biashara ya muda mfupi kwa kuuza haraka na kupata faida kwa haraka. Biashara ya muda mfupi au yenye faida ya haraka ni  kama kamari.  Badala yake, jifunze kuwekeza kwa muda mrefu. Chagua biashara nzuri, weka msingi thabiti katika hiyo biashara. Hepuka marafiki wanaokuambia biashara Fulani inalipa alafu wao hawaifanyi, fanya biashara ambayo wewe unaipenda.
3.      Nunua hisa.
Watu wengi hawana elimu ya kutosha katika soko la hisa. Ukinunua hiza katika makampuni au taasisi, hisa zako zitakua na kuleta faida baadae. Kwa mfano Airtel wamekubali kuuza hisa zake nchini ni moja ya fursa ya kuchangamkia. Kuapata taarifa zaidi tembelea tofutti ya soko la hiza Tanzania.

Takwimu zinaonesha  kwamba watu wachache wanahifadhi pesa za kutosha kwa ajili ya kustaafu au maisha ya uzeeni. Ila wengine wanahisi kuwa hawawezi kamwe kustaafu au kuzeeka.kipindi ambacho bado una nguvu za kutosha wekeza katika kuandaa maisha yako ya baadae ili usije ukawa mzee masikini. Unaweza kufanya yafuatayo:-
i)                    Kusomesha watoto
ii)                  Kujenga nyumba imara
iii)                Kununua maeneo yanauzwa kwa bei nafuu.
iv)                Kuhifadhi pesa benki.
v)                  Kufungua biashara endelevu. nk
Mali isiyohamishika kama nyumba ya kupangisha au kiwanja katika eneo linalo kuwa kwa kasi ni njia nzuri ya kujenga utajiri.  Watu wengi, hata hivyo, wamefanya vizuri sana katika uwekezaji katika mali isiyohamishika. 
6.      Wekeza muda wako. 
Kwa mfano, unapokuwa na  na muda wa bure, tenga saa chache kufanya kitu. Lakini ukiamua kuwa tajiri fanya kazi hadi saa 15 kwa siku.  
Kutumia 15,000,000 kwenye gari wakati mwingine ni upotezaji wa fedha, kwa sababu inawezekana baada tu yakuinunua  haitakuwa na thamani ya hela uliyoinunulia. Unapoiendesha gari mpya kwenye barabara inapungua dhamani kwa 20% -25% na inaendelea kufanya hivyo kila siku. 
8.      Usitumie pesa kwenye mambo ya kijinga. 
Usikubali kutumia fedha zako ngumu kwenye mambo ya kijinga. Jiepushe na michezo ya kubahatisha mfano. 
-       Casino na tiketi za bahati nasibu. Kwani wachache hupata bahati ya kushinda lakini waliowengi hupoteza.
-       Uvutaji sigara . Wanaovuta sigara wanaweza kutazama pesa zao tu kwenye moshi wa sigara.
-       Huwanywaji wa pombe uliopitiliza

NJIA YA PILI: TAJIRIKA KUPITIA KUFANYA KAZI
1.      Jiongeze  kitaaluma.

 Kupitia kujiongeza kitaaluma kutakufanya kupanda kuongeza ufanisi katika ufanyaji wako wa kazi. Hivyo unaweza kuongezewa kiwango cha mshahara pamoja na kupanda cheo. 
2.      Chagua taaluma sahihi . 
Kama haujasomea kazi au unataka kujiongeza kitaaluma angalia tafiti za mishahara ambazo zinaonyesha mapato ya wastani ya kila mwaka kwa fani maalum. Vigezo  vyako vya kupata utajiri vitapungua ikiwa utasomea kazi yenye kipato kidogo. Hapa ni baadhi ya ajira zinazolipa zaidi. Kwa mfano taaluma za Udaktari, Uhandisi wa petrol na gesi, sheria, utunza fedha, siasa, Tehama n.k  wana nafasi kubwa ya kuwapata fedha nyingi, wanaweza kuingiza zaidi ya Tsh 30,000,000 kwa mwaka.
3.      Chagua eneo sahihi . 
Nenda kafanye kazi sehemu/eneo zuri lenye fursa.  Kuna fursa nyingi zaidi katika miji mikubwa kuliko maeneo ya vijijini, vijijini kunaweza kuwa sehemu ya kuanzia, ukitaka kufanya kazi pamoja na biashara, nenda kafanye kazi katika miji yenye watu wengi.
Omba kazi maeneo mengi na ujishughulishe na mahojiano mengi. Unapopata kazi, ifanye kwa juhudi  ilikupata uzoefu na kupanda vyeo. Kazi ambazo hazina nafasi za kupanda hazimpi mtu motisha ya kufanya kazi na umkosesha kipato.

5.      Badilisha ajira na mwajiri . 
Mara tu upatapo uzoefu kwenye fan/kazi yako, fikiria kupata kazi mpya au majukmu mapya. Hii itakufanya kubadilisha mazingira yako kazi, unaweza kuongeza kipato chako na uzoefu wa tamaduni tofauti za ufanyaji kazi. Usiogope kufanya hivyo mara kadhaa. Ikiwa wewe ni mfanyakazi wa thamani, pia inawezekana kuwa kampuni/taasisi yako ya sasa inaweza kukupa faida (kukuongezea malipo) au faida nyingine yoyote  ikiwa wanajua unataka kuondoka.
NJIA YA TATU: KUPUNGUZA GHARAMA ZA MAISHA
1.      Jifunze kuhifadhi chakula na mahitaji mengine . 
Ukiwa na ziada ya chakula ndani itakusaidia kuweka akiba kutoka katika vipato vyako. Kuliko kila siku unanunua mahaji. Nunua jokovu hifadhi chakula kinacho baki hii ni hazina ya siku nyingine.
Umeme, gesi, na huduma zingine zinaweza kuathiri bajeti yako ya kila mwezi ikiwa vitatumika vibaya. Mfano taa zote ndani ya nyumba kuwashwa kwa wakati mmoja alafu baadhi ya maeneo hamna mtu, kupika chakula kingi na kulazimisha kukimaliza, kuchemsha maji ya kuoga baadala ya kufanya mazoezi kisha ukaoga maji ya kawaida nk. Kwahiyo shusha bili zako na utafakari kabla ya kulipia bili mbali mbali.
NJIA YA NNE: KUOKOA FEDHA
1.      Jilipe kwanza . 
Hii inamaanisha kabla ya kwenda kutumia mshahara wako au kipato chako weka pesa katika akiba yako, unaweza kuweka kwenye kibubu au akaunti au kwenye mtandao wa simu. Fanya hivi kila wakati unapolipwa mshahara au kupata kipato chochote na uhakikishe akiba yako inakua.
2.      Panga bajeti yako
Tengeneza  bajeti ya kila mwezi ambayo inhusu gharama zako zote za msingi na acha hela kidogo kando ya kustarehe/kujiburudisha/dharura. Zingatia bajeti yako ilikuokoa fedha angalau kila mwezi nah ii ni mmoja ya  jitihada  za kuwa tajiri.
3.      Punguza gharama katika usafiri na makazi . 
Hivi, ungependa kuwa na ghorofa badala ya nyumba ya kawaida ? Je ni lazima kununua usafiri badala ya kutumia usafiri wa kawaida? Kuna haja ya kujenga nyumba yako ikiwa gharama za kupanga nyumba ziko chini? Je! Unaweza kununua gari ambalo limetumika badala ya mpya na kuitumia kwa upole? Haya ni maswali ambayo unatakiwa kujiuliza ili  kuhifadhi tani ya fedha kila mwezi.
4.      Kata gharama .
 Angalia njia ambazo hutumia fedha nyingi kisha tafakari. Kwa mfano, nunua vitu siku za minada ambapo gharama zinakuwa chini. Pia nunua vitu original ili vitumike kwa muda mrefu badala ya kila siku unanunua kitu ambacho ulishawahi kukinunua.
5.      Achana  mikopo isiyokuwa na ulazima . 
Lipa bei  kamili kwa wakati ili kukwepa riba isiyo na ulazima. Kwa mfano kukopa vocha ya shilingi 600 kisha unalipa 700 ukijumlisha na riba ya shilingi 100.
Bottom of Form